Thiago Alcantara amefunga mabao matatu kipindi cha kwanza kuipa ushindi Hispania
KIUNGO
Thiago Alcantara amekuwa kivutio katika ushindi wa kikosi cha vijana cha
Hispania chini ya miaka 21 wa mabao 4-2 dhidi ya Italia na kutwaa Kombe
la Ulaya kwa vijana barani humo, baada ya mchezaji huyo anayetakiwa na
Manchester United kufunga mabao matatu mjini Jerusalem.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 wa Barcelona amekuwa akihusishwa kwa kiasi kikubwa na kuhamia Old Trafford.
Alcantara,
aliyekuwamo kwenye kikosi cha Hispania kilichoshinda taji hilo miaka
miwili iliyopita nchini Denmark, aliifungia timu yake bao la kwanza
dakika ya sita, lakini Italia ikasawazisha haraka kupitia kwa Ciro
Immobile dakika ya 10.
Thiago
akafunga tena dakika ya 31 na 38 kwa penalti, kabla ya Isco kufunga
dakika ya 66 kwa penalti pia na Borini akaifungia Italia dakika ya 79
kufanya 4-2.
Kikosi
cha Hispania leo kilikuwa; De Gea, Montoya, Bartra, Martinez, Moreno,
Koke/Camacho dk86, Illarramendi, Thiago, Tello/Muniain dk70,
Morata/Rodrigo dk80 na Isco.
Italy
U21; Bardi, Donati, Bianchetti, Caldirola, Regini, Florenzi/Saponara
dk58, Rossi, Verratti/Crimi dk76, Insigne, Borini na Immobile/Gabbiadini
dk58. Chanzo: sportmail
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment