Stori:Musa Mateja
STAA
wa filamu za Kibongo aliyebarikiwa kipaji cha kuigiza sauti za watu
mashuhuri, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amesema ugonjwa uliompata
unamtesa sana.Akizungumza na mwandishi wetu Jumatatu iliyopita nyumbani
kwake, Kinondoni jijini Dar, Steve alisema anasumbuliwa na mkono wa
kulia ambao umevimba na kutoa maji kiasi cha kumfanya usiku asiweze
kupata usingizi mpaka achome sindano.
“Mkono
umevimba, unatoa majimaji kama vile nimeungua na moto na mifupa
inaniuma sana kiasi cha kushindwa kufanya shughuli zangu,” alisema.
Staa
huyo alimwambia mwandishi wetu kwamba chanzo cha ugonjwa huo ni maralia
iliyompata na kwenda hospitali ambako aliandikiwa dawa mseto.
“Nilitumia dozi ya kwanza, kisha ya pili hapo ndipo tatizo lilipoanza, hospitali wanasema nina aleji,” alisema.
Hali hiyo imemfanya Steve kudhoofu na muda mwingi kushinda ndani kwa
takribani wiki mbili sasa kwa kuwa mifupa ya mkono huo inamuuma sana
hususan usiku unapoingia.
Aidha, Steve amewashukuru mastaa wenzake wanaompa sapoti kwa
kumtembelea na kumjulia hali na akawataja wachache kuwa, ni Jacob Steven
‘JB’, Vincent Kigosi ‘Ray’ Mama Rolaa na Sabrina Rupia ‘Cathy’.
CHANZO : GLOBAL PUBLISHER
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment