BAADHI ya wasanii wa filamu Bongo
wamemtaka mwenzao, Kajala Masanja (pichani) kuwa mkweli kuhusiana na
ushosti wake na Wema Sepetu kwani kudai kwamba wako sawa wakati ukweli
unajulikana ni unafiki.
Wakizungumza na Ijumaa juzikati,
baadhi ya wasanii hao walioomba majina yao yasiandikwe walisema
wameshangazwa na maneno ya Kajala kwenye mtandao kuwa hana tatizo na
Wema wakati wao wanajua wametofautiana.
“Mlipoandika kuwa Wema na Kajala
wametibuana sikushangaa kwani ndiyo ukweli lakini nikaona kwenye mtandao
Kajala anasema eti yuko sawa na Wema, aache unafiki, awe mkweli
tumsaidie maana sisi tunamjua vizuri Wema. Ili uwe rafiki yake ufunge
mkanda,” alisema mmoja wa wasanii hao ambaye pia ni rafiki wa karibu wa
Kajala.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment