KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa
filamu na muziki Baby Joseph Madaha amejikuta katika wakati mgumu baada
ya kuibiwa nguo zake za ndani alizokuwa ameanika nje maeneo ya Mikocheni
jijini Dar.
Chanzo cha habari ambacho ni shosti wa karibu wa mwanadada huyo kilichoomba hifadhi ya jina lake kilitiririka:
“Alizifua kama dazeni nzima hivi na
kuzianika nje kisha kwenda kwenye mishe zake. Heh! Kumbe vibaka hawaachi
kitu, waliruka fensi wakazichukua pamoja na ndala.”
Katika kujua ukweli wa habari hizo,
mwandishi wetu alimtafuta Baby Madaha na alipopatikana alisema ni kweli
alilizwa nguo hizo na kudai anafanya jitihada za kuhama kwani eneo
analoishi limezidi kwa wizi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment