Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

NDOA ZA JINSIA MOJA ZAANZA TENA CALIFORNIA BAADA YA MARUFUKU KUONDOLEWA

*Obama asema ni "ushindi kwa demokrasia ya Marekani.

Mashoga na wasagaji katika jimbo la California walitimka kwenda kufunga ndoa baada ya marufuku ya ndoa za jinsia moja kuondolewa katika jimbo hilo. Marufuku hiyo iliyoondolewa iliwekwa mwaka 2008.

Jana Ijumaa, mahakama ya Rufaa ya Marekani ilitoa uamuzi kuwa ndoa za jinsia moja zinaweza kuanza upya katika jimbo la California.

Kwa mujibu wa sheria, mahakama hiyo ilitakiwa kusubiri kwa muda wa siku 25 kabla ya kuiondoa marufuku hiyo.

Mara tu baada ya tangazo hilo la kushtukiza, ndoa zilianza kufungwa katika ukumbi wa jiji, ikiwa ni miaka minne baada ya wapiga kura kupitisha marufuku hiyo katika jimbo hilo.

Ruhusa hiyo inakuja siku mbili baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kwamba wanandoa wa jinsia moja wanaweza kupata mafao kama wanandoa wengine na kuondoa marufuku ya ndoa za mashoga katika jimbo la California.

Hukumu hiyo ya Jumatano iliyotolewa na mahakama kuu ilivunjilia mbali Sheria ya Ulinzi wa Ndoa au Defense of Marriage Act (DOMA) iliyotafsiri ndoa kuwa ni muungano wa mwanaume mmoja na mwanamke mmoja.

Ndoa za jinsia moja ni kinyume na silika ya maumbile ya mwanadamu na inapingana na mafundisho ya dini zote za kiroho zinazoeleza kuwa ndoa ni muungano wa mwanamke na mwanaume.
 
Siku ya alhamisi Rais Barack Obama alisema kuwa uamuzi huo wa mahakama ni “ushindi kwa demokrasia ya Marekani”.
 
Kwa sasa ndoa ya jinsia moja imeruhusiwa katika majimbo 13 ya Marekani na katika Mkoa wa Columbia.

http://mzizima-24.blogspot.com/2013/06/ndoa-za-jinsia-moja-zaanza-tena.html
*Obama asema ni "ushindi kwa demokrasia ya Marekani.

Mashoga na wasagaji katika jimbo la California walitimka kwenda kufunga ndoa baada ya marufuku ya ndoa za jinsia moja kuondolewa katika jimbo hilo. Marufuku hiyo iliyoondolewa iliwekwa mwaka 2008.

Jana Ijumaa, mahakama ya Rufaa ya Marekani ilitoa uamuzi kuwa ndoa za jinsia moja zinaweza kuanza upya katika jimbo la California.

Kwa mujibu wa sheria, mahakama hiyo ilitakiwa kusubiri kwa muda wa siku 25 kabla ya kuiondoa marufuku hiyo.

Mara tu baada ya tangazo hilo la kushtukiza, ndoa zilianza kufungwa katika ukumbi wa jiji, ikiwa ni miaka minne baada ya wapiga kura kupitisha marufuku hiyo katika jimbo hilo.

Ruhusa hiyo inakuja siku mbili baada ya Mahakama Kuu kutoa uamuzi wa kwamba wanandoa wa jinsia moja wanaweza kupata mafao kama wanandoa wengine na kuondoa marufuku ya ndoa za mashoga katika jimbo la California.

Hukumu hiyo ya Jumatano iliyotolewa na mahakama kuu ilivunjilia mbali Sheria ya Ulinzi wa Ndoa au Defense of Marriage Act (DOMA) iliyotafsiri ndoa kuwa ni muungano wa mwanaume mmoja na mwanamke mmoja.

Ndoa za jinsia moja ni kinyume na silika ya maumbile ya mwanadamu na inapingana na mafundisho ya dini zote za kiroho zinazoeleza kuwa ndoa ni muungano wa mwanamke na mwanaume.

Siku ya alhamisi Rais Barack Obama alisema kuwa uamuzi huo wa mahakama ni “ushindi kwa demokrasia ya Marekani”.

Kwa sasa ndoa ya jinsia moja imeruhusiwa katika majimbo 13 ya Marekani na katika Mkoa wa Columbia 
na mzizima24.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

Top