Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jessica-Cambensy-and-Jaycee-Chan-in-Double-Trouble-2012-Movie-ImageJacee Chan mwana wa mwana nyota wa filamu Jackie Chan amehukumiwa kifungo cha miezi sita jela kwa kutumia mihadarati.
Chan mwenye umri wa miaka 32 alikiri kufanya makosa hayo katika mahakama ya wiliaya ya mjini Beijing Dongcheng kwa kuwaficha wengine ili kutumia dawa za kulevya.
Polisi walivamisa nyumba yake mnamo mwezi Agosti na kupata gramu 100 za marijuana.
Alikabiliwa na hukumu ya miaka mitatu.
Kukamatwa kwake kunajiri kufuatia msako wa dawa za kulevya nchini Uchina ambapo watu kadhaa mashuhuri walikamatwa.
Jacee Chan na babaake jackie Chan
Mnamo mwezi Juni mwaka 2014,rais Xi Jinping aliwaagiza polisi kutumia mikakati mikali ili kusitisha utumizi wa mihadarati.
Kukiri kwa mwana wa mcheza filamu mashuhuri nchini Uchina kunatoa ujumbe muhimu kutoka kwa serikali ya Uchina.
Hakuna aliye na kinga nchini Uchina katika msako huo wa dawa za kulevya.
Chan na nyota wa filamu kutoka Taiwan Kai Ko mwenye umri wa miaka 23 walikamatwa pamoja katika nyumba ya Beijing mnamo mwezi Agosti huku polisi wakisema kuwa walipatikana wametumia bangi.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top