Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
IMG_0504.JPG
Siku moja baada ya Kagera Sugar kuishushia kipigo Simba katika Uwanja wa Taifa, ligi kuu ya Tanzania bara maarufu kama Vodacom Premier League imeendelea tena jioni hii kwa mchezo kati ya Yanga SC vs Azam FC.
Katika mchezo huo uliopigwa katika Uwanja wa Taifa, Azam ilikuwa ya kwanza kupata bao alilofunga na Didier Kavumbagu dakika 6, Yanga walisawazisha kupitia Amiss Tambwe (7) na kupata la pili lililofungwa na Simon Msuva (57), kabla ya John Boccoaliyeingia akitoa benchi kuisawazishia Azam dakika 65.
Kwa matokeo hayo Yanga imefikisha pointi 14, sawa na Azam, wakati Mtibwa Sugarimebaki kileleni ikiwa na pointi 16, baada ya kulazimishwa sare 1-1 na Stand United jana asubuhi mchezo huo juzi ilivunjwa kutokana na mvua kubwa kunyesha.
John Bocco aliifungia Azam Fc bao la kusawazisha baada ya kuingia akitokea benchi .
John Bocco aliifungia Azam FC bao la kusawazisha baada ya kuingia akitokea benchi.
Mbeya City imejiondoa mkiani baada ya kuichapa Ndanda FC 1-0, wakati Polisi Morogoro imeinyuka Mgambo JKT kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri.
Kutoka MorogoroPolisi Morogoro wameutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Mgambo JKT kwa mabao 2-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Polisi ilipata bao kwanza dakika 22, lililofungwa na Nicolaus Kabipe kabla ya Iman Mapunda kupachika bao la pili kwa kichwa dakika 85, akiunganisha kona ya Kabipe.
Kutoka MbeyaDeus Kaseke aliwainua mashabiki wa Mbeya City dakika pili kwa kufunga bao pekee akiunganisha kwa shuti lililomshinda kipa wa Ndanda FCSalehe Marande na kujaa wavuni.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top