Taarifa kutoka Dodoma na kuthibitishwa na Polisi, zinahusu Wananchi kupatwa na hasira na kumuua Mwanaume aliyemuua mke wake kwa kumpiga na rungu tumboni kwenye kijiji cha Mzogole.
Mwanamke aliyeuwawa ana umri wa miaka 48 Mwajuma Chomola na mume wake ambae ndio mtuhumiwa ana umri wa miaka 55 anaitwa Richard Kodi ambapo kwa mujibu wa gazeti la HabariLEO, Mwanaume huyu alifariki dunia wakati akihudumiwa hospitali ya wilaya ya Mpwapwa.
Wakati uchunguzi ukiendelea, matokeo ya awali yanaonyesha chanzo cha yeye kumuua mke wake waliekua wakiishi pamoja ni wivu wa kimapenzi na kwamba ishu ilianzia pale Mwanamke alipochelewa kurudi nyumbani akitokea kwenye sherehe iliyofanyika kwenye kijiji hichohicho wanachoishi lakini mume alidhani mke kaenda kwengine.
Yaani sio kwamba alimfumania bali alihisi tu mke wake kaenda kwengine ndio sababu iliyomfanya akachukua haya maamuzi, mara nyingi kwenye mapenzi kumekua na kesi nyingi zinazosababisha Wanawake kupigwa au kuuwawa kwa sababu tu Mwanaume anahisi vitu kama hivi bila kuwa na ushahidi.
Bonyeza hapa
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment