RAIS wa Bongo Movie Unit,
Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ amemmwagia sifa staa wa filamu Bongo,
Elizabeth Michael ‘Lulu’ kuwa ni binti mdogo lakini sasa anajitambua
tofauti na wasanii wengine wakubwa.
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Akipiga stori na Ijumaa Steve alisema kuwa, mbali na umakini katika
kazi zake za kisanii, sasa hivi yuko makini sana na maisha yake kiasi
kwamba ni nadra sana kumkuta na skendo za kijingajinga.
Steve Nyerere.
“Achilia mbali hao mastaa wote unaowajua wewe, mimi nikiwa kama
kiongozi wa Bongo Movie siwezi kusema uongo, namkubali sana Lulu kwani
ni binti mdogo na anajitambua na sasa siyo mtu wa kuendekeza mambo ya
starehe kama wengine, pia huwezi kumuona viwanja kirahisi, katulia
anafanya kazi,” alisema rais huyo.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






Post a Comment
Post a Comment