Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Zuwena Mohamed ‘Shilole’. 

MWANAMUZIKI wa miondoko ya mduara ambaye pia ni msanii wa filamu, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ amefunguka kuwa kwa alichokiona, amekoma kutumia mkorogo.

Akipiga stori na Ijumaa, Shilole alisema mwanzo alikuwa akitumia mkorogo aina ya ‘karolaiti’ lakini amegundua badala ya kumfanya awe mzuri zaidi, umemletea
matatizo kwenye mwili wake.
“Niseme tu kwamba nimekoma na ningejua nisingefanya jaribio la kujichubua, nimeathrika sana na sijaona faida yoyote, zaidi umeniharibia ngozi yangu,” alisema Shilole na kuongeza:

“Imefika wakati natamani niirudishe ile ngozi yangu ya asili lakini siwezi, sasa hivi nikiumia kidonda kinachukua muda mrefu kupona sababu ya huu 
mkorogo, warembo wanaojipenda ni bora wakaachana na mambo hayo.

Bonyeza Hapa like page yetu

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top