Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
KLABU ya Real Madrid imeifumua Deportivo la Coruna mabao 8-2 katika La LIga Uwanja wa Riazor jioni hii, Cristiano Ronaldo akipiga hat-trick yake ya 23 kwa Los Blancos.

Ronaldo alifunga mabao yake katika dakika za 29, 41 na 78, wakati mabao mengineya Real yamefungwa na James Rodriguez dakika ya 36, Gareth Bale dakika ya 66 na 74 na Javier Hernandez ‘Chichairto’ dakika ya 88 na 90.

Deportivo ilipata mabao yake ya kufutia
machozi kupitia kwa Haris Medunjanin na Jose Verdu Nicolas.

Kikosi cha Real kilikuwa: Casillas, Arbeloa, Ramos, Varane, Marcelo, Modric/IIaramendi, Kroos, Bale/Hernandez, James, Ronaldo na
Benzema/Isco.

Deportivo: Lux, Laure, Diakite, Sidnei,
Luisinho, Bergantiños, Medunjanin, Juanfran/ Juan Dominguez, Farina/Toche, Cuenca na Postiga/Cavaleiro.
Bonyeza Hapa like page yetu 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top