Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ukweli haufichiki daima labda kuuchelewesha tu! Ndicho kinachomkuta muigizaji wa kike wa filamu ya ‘Django Unchained’ wa Marekani, Daniele Watts aliyewapa wakati mgumu polisi wa Los Angeles kwa kuwatuhumu kumnyanyasa na kumfanyia ubaguzi wa rangi alipokuwa na mpenzi wake Brian James.Picha: Muigizaji mkubwa aliyedai amenyanyaswa na polisi, alikutwa akifanya mapenzi kwenye gari, Picha ziko hapa
Awali Daniele alisababisha matatizo kwa polisi hao baada ya kuonekana katika picha akiwa analia mbele ya polisi hali iliyoaminika kuwa alikuwa anaonewa.
Lakini TMZ wamepata picha na ushahidi kutoka kwa shuhuda wa tukio hilo ambaye ameeleza kuwa aliwaona Daniele na mpenzi wake Brian wakiwa katika harakati za kufanya mapenzi kwenye gari.
Picha hizo zilizochukuliwa katika eneo la tukio siku ya Alhamisi zinaomuonesha Daniele na Brian wakiwa wameegesha gari, mlango mmoja ukiwa wazi wakifanya kilichokatazwa kisheria.
Inaelezwa kuwa mtu mmoja aliyeliona tukio hilo aliwaita polisi na kila kitu kiliwekwa wazi muda huo.
Katika sauti iliyonaswa na TMZ, muigizaji  huyo anasikika akiwasumbua polisi hao kwa maneno na kutumia 'F-Word' kwenye sentensi zake.
Katika sauti nyingine iliyonaswa na Mail Online, Daniele anasikika akimwambia polisi aliyemfunga pingu kuwa anajua haki zake kutokana na uzoefu alioupata katika uigizaji.
Daniele Watts alicheza uhusika wa poliso katika comedy ya ‘Weeds’ ya mwaka 2012.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top