![]() |
Bidhaa mbalimbali za madukani zikiwa tayari kwaaajili ya kuteketezwa baada ya muda wake wa matumizi kuisha,kufuatia msako wa kushitukiza wa TFDA.
Na Editha Karlo - Kigoma
Bonyeza Hapa like page yetu Zaidi ya Tani 24 za vyakula,dawa za binaadam na vipodozi zimeteketezwa na mamlaka ya chakula na dawa(TFDA)katika mikoa minne ya kanda ya katikwasababu ya kutofaa kwa matumizi ya binaadam. Akizungumza wakati wa zoezi la uteketezaji wa bidhaa hizo zilizokamatwa katika zoezi la kustukiza ndani ya Manispaa ya Kigoma ujiji Mkoani Kigoma, Mkaguzi wa TFDA kanda ya kati Bw.Engliber Bilashoboka alisema kuwa bidhaa hizo zilikamatwa kati ya Julai mwaka jana (2013 ) na Juni mwaka huu (2014). Bw. Bilashoka alisema kuwa kuteketezwa kwa bidhaa hizo kunatokana na ukaguzi unaofanywa na maofisa wa TFDA katika mikoa mbalimbali nchini na lengo likiwa ni kuondoa sokoni bidhaa zilizoisha muda wake na zisizofaa kwa matumizi ya bindaadam Alisema pia kufuatia zoezi hilo mamlaka yake imekifungia kiwanda cha mikate cha Kigoma bekari baada ya kukutwa na tani 1.5 za mikate mibovu, pamoja na machinjio ya ujiji kwa kufanya shughuli zake katika hali inayotishia afya za wananchi Alisema bidhaa hizo zimekamatwa katika mikoa ya Tabora,Kigoma,Singida na dodoma alisema kuwa katika bidhaa zilikamatwa na kuteketezwa nyingi zilikuwa zikiuzwa huku muda wake wa kuwa sokoni ukiwa umeisha na zingine zimepigwa marufuku kuuzwa nchini. Ofisa huyo alisema kuwa uteketezaji katika manispaa ya kigoma kwa muda wa wiki moja mpaka sasa ,alisema mamlaka ya ke imeteketeza zaidi ya tani 4.1zenye thamani ya shilingi milioni 24 ambavyo havifai kwa matumizi ya binaadamu Naye Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Moses Welansari akizungumzia zoezi hilo alisema kuwa wamekuwa wakikutana changamoto za wenye maduka zilizokatazwa au zilizoisha muda wake wa matumizi. ''Elimu imekuwa ikitolewa kwa wafanyabiasha mara kwa mara ili kuepuka kuweka sokoni bidhaa zisizotakiwa na mamlaka za serikali na zilizoisha muda wake ''alisema Kaimu Mkurugenzi. |
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro






.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment
Post a Comment