Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Stori: Gladness Mallya

MSANII wa filamu ambaye pia ni mweka hazina msaidizi wa klabu ya Bongo Movie Unity, Sabrina Rupia ‘Cathy’ amefunguka kwamba anaona kundi hilo linakwenda kufa na halitakuwepo kabisa kutokana na kujiuzulu kwa mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.



Akistorisha na paparazi wetu, Cathy alisema amejisikia vibaya Steve Nyerere kujiuzulu na wao kama viongozi hawakuwa na taarifa hivyo kutokana na kwamba kiongozi huyo alikuwa mpiganaji Bongo Movie itakufa kwani hakuna mtu anayeweza kuongoza kama Steve.

“Steve yeye kama binadamu ana mapungufu kidogo lakini mazuri aliyofanya ni mengi kwani alikuwa mpenda maendeleo lakini kujiuzulu kwake ni pigo na ninaona kama kundi hili halitakuwepo tena, yaani ninajisikia vibaya sana na amejiuzulu ghafla mno,” alisema Cathy.
GPL

Bonyeza Hapa like page yetu 

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top