![]() |
|
Baadhi ya samaki wanaweza kukumbuka mazingira
yao kwa muda wa wiki mbili
Watafiti hao wanasema ongezeko hilo la muda wa
samaki kukumbuka, huenda likampa samaki nafasi ya kuishi zaidi hususan wakati
kuna upungufu wa chakula.
"Samaki wanaoweza kukumbuka mahali
chakula kilipo, wana uwezo wa kuishi zaidi kuliko wale ambao hawakumbuki,"
alisema mwandishi mwenza wa ripoti ya utafiti huo Trevor Hamilton, ambaye ni
mwanasayansi wa chuo hicho kikuu cha MacEwan nchini Canada,
Alisema samaki wanaweza kukumbuka kwamba
sehemu maalum ina chakula bila kuwepo tishio la samaki wanaoweza kuwaua, na
hivyo wataweza kurudi tena katika sehemu ile.
Wanasayansi hao wanasema samaki wakiwa
baharini, ni muhimu waweze kutambua maeneo yalio na chakula ili waweze
kuendelea kuishi.
Chanzo:- BBC Swahili
kama huja like ukurasa wetu wa facebook fanya hivi sasa ili habari ziwe zinakuijia punde tu zinapoweka kwenye mtandao huu BONYEZA HAPA
|
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment