Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Leo hii jumapili tarehe 23/3 watu kadhaa
ambao wanasadikika kuwa ni magaidi
wamevamia kanisa moja linalojulikana kwa
jina la Joy Jesus Church huko Mombasa na
kuanza kupiga risasi kanisani
hapo.Mashuhuda wa tukio hilo wanasema
baada ya watu hao kutekeleza tukio hilo
walikimbia kwa miguu kuelekea pasipo
julikana.Afisa wa polisi wa eneo hilo
amesema hadi sasa wamefariki watu wawili
na wengine kumi wamepata majeraha ya
risasi nakukimbizwa hospitali.
Kikundi cha Al Shabaab kiliwahi kuhusishwa
na tukio kama hili huko Nairobi lakini hivi
sasa limetokea Mombasa.
Maafisa wa polisi wamesema wanaendelea
kufanya uchunguzi wa kuwakamata watu hao
japokuwa hadi sasa bado hawajapata tetesi
yoyote juu ya watuhumiwa hao

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top