Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa
Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa
mtaliiBi. Jeanne Traska (32) kutoka
Ujerumani pamoja na muongoza wageni
Athuman Juma ambao jana walikwama katika
kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro.
Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza
kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa
kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa
kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja
jioni.
Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na
mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha
Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na
hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha
kuwapeleka katika kituo cha Horombo
majira ya saa mbili usiku ambapo
walichukuliwa na gari kupitia njia maalum
ya uokoaji na kufika katika Lango Kuu la
Marangu saa nne na nusu usiku.
Hali ya hewa ilisababisha helikopta
maalum iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la
uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa
kuwa mawingu mazito hayakuwezesha
marubani kuliona eneo la kilele kwa urahisi.
Hivi sasa mtalii huyo pamoja na muongoza
wageni wake bado wapo chini ya uangalizi
wa hifadhi kwa kushirikiana na Kampuni ya
Nordic Tours iliyomleta mgeni huyo.
Aidha, kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida,
uongozi wa hifadhi unaendelea kuchunguza
sababu zilizowafanya kuchepuka njia na
kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo.
Kwa kawaida Kilele cha Mawenzi huwa
hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza
fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni
amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele
hicho.
Imetolewa na
Idara ya Mawasiliano
Hifadhi za Taifa
Tanzania
23.03.2014
picha hapo chini ni Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na
Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa
katika Lango la Marangu pamoja na vifaa
mbalimbali walivyokwama navyo katika
kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro
mara baada ya kuokolewa.






Post a Comment
Post a Comment