Maelfu
ya waandamanaji wameingia barabarani mjini Paris hii katika maadhimisho
ya mwaka mmoja wa kuwa madarakanai Rais Francois Hollande (pichani)
wakimshutumu kwa kuupa kisogo siasa za mrengo wa kushoto.
Katika
mkesha wa kuadhimisha ushindi wa Hollande wa Mei 6 mwaka jana dhidi ya
aliyekuwa rais wa siasa za mrengo wa kulia Nicolas Sarkozy, upande wa
siasa za mrengo wa kushoto unaoungwa mkono na viongozi wa Kikomunisti
wamewakusanya wafuasi wao kwa maandamano kunzia Bastille, ambao ni
ukumbi maarufu katika vuguvugu la mapinduzi ya Ufaransa.
Watu
wengi pia walitarajiwa kufanya maandamano tofauti mjini Paris na miji
mingine ya kuipinga mipango ya serikali ya kuidhinisha ndoa za jinsia
moja na kuwaruhusu mashoga kuwalea watoto.
Maandamano
hayo yanakuja wakati uchunguzi wa maoni ukionesha kuwa Hollande ndiye
rais asiyependwa na raia wengi wa nchi hiyo katika historia ya
karibuni-
chanzo:DW
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment