Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Watu wanane wakiwemo raia wa Saudi Arabia wamekamatwa nchini Tanzania, kuhusiana na shambulio lililofanyika dhidi ya Kanisa moja wakati wa ibada ya Jumapili jijini Arusha, ambapo watu wawili waliuawa. Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ameliita shambulio hilo kuwa ni la kigaidi, lililofanywa na mtu au kundi la watu wakatili, ambao ni maadui wa nchi hiyo. Watu wengine wasiopungua 30 walijeruhiwa katika shambulio hilo, ambalo ni la kwanza la ukubwa huo kulilenga kanisa.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amesema wasaudi wanne waliokamatwa kuhusiana na shambulio hilo waliwasili katika uwanja wa ndege wa Arusha siku ya Jumamosi, na kwamba Watanzania wanne waliokamatwa ni wakristu, lakini hakutoa maelezo zaidi. Balozi wa Vatican nchini Tanzania Francisco Montecillo Padilla, alikuwa akihudhuria misa katika kanisa hilo ambalo limejengwa upya, lililoko katika viunga vya jiji la Arusha, lakini hakudhuriwa.
Maafisa hawajatoa ishara zozote kuhusiana na nani aliefanya shambulio hilo, lakini wasiwasi umekuwa ukiongezeka kati ya jamii za Wakristu na Waislamu katika miezi ya hivi karibuni. Rais Kikwete amewataka Watanzania kuwa watulivu wakati polisi ikiendelea na uchunguzi wake.
chanzo:dw

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top