MWALIMU Daniel Msalika (42) wa shule ya msingi Nyasosi, wilayani Bariadi, mkoa wa Simiyu amefariki dunia katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando alikokuwa amelazwa akitibiwa majeraha.
Majeraha hayo yalitokana na kushambuliwa na baadhi ya wananchi kwa madai ya kujihusisha kimapenzi na wanafunzi wa kike wa shule hiyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Onesmo Lyanga aliwaeleza waandishi wa habari jana ofisini kwake kuwa mwalimu huyo alifariki dunia Julai 31 mwaka huu saa nane usiku.
Kamanda Lyanga alisema kuwa siku ya tukio Julai 27 mwaka huu saa 6.30 usiku, wananchi hao ambao idadi yao haijafahamika, walivamia nyumba ya mwalimu huyo baada ya kupata taarifa kuwa kuna mwanafunzi ambaye amelala nyumbani kwake, jambo ambalo halikuwa la kweli.
“Wananchi hao walipata taarifa ya kuwa nyumbani kwa mwalimu kuna mwanafunzi ambaye amelala humo hivyo walimvamia kwa kuvunja mlango na kuanza kumshambulia kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi na kumsababishia majeraha makubwa sehemu za kichwani na usoni lakini binti waliyemkuta kwake ni mwenye umri wa miaka 18 na siyo mwanafunzi,” alisema.
Alisema kuwa baada ya uvamizi huo, mwalimu huyo alikimbizwa katika Kituo cha Afya cha Isanga kupatiwa matibabu, lakini hali yake iliendelea kuwa mbaya na kupelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza, lakini alifariki dunia.
Kamanda alisema kifo chake, kimesababishwa na majeraha ya kushambuliwa huku tuhuma dhidi yake zikiwa si za kweli.
Alitoa mwito kwa wananchi kuacha kujichukulia sheria mikononi huku wakisisitiza kuwa wote watakaobainika kusababisha kifo hicho, sheria itachukua mkondo wake.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Uteuzi mwingine wa Rais Magufuli leo September 9 201609 Sep 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo September 09 201...Read more ?
- Viongozi wa Afrika Mashariki Waigomea Ulaya....Wajipa Miezi Mitatu Kuutafakari Mkataba wa EPA09 Sep 20160
JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC), imeiomba Jumuiya ya Ulaya (EU), iipe muda wa miezi mitatu kuju...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Majibu ya Waziri mkuu Majaliwa Leo Bungeni kuhusu wahusika wa mauaji ya askari08 Sep 20160
Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inaendelea kukutana na wadau tofauti wanaohusika na ...Read more ?
- Makamu wa Rais: Viongozi Na Watumishi Wa Umma Kuchukuliwa Hatua Kali Iwapo Watabainika Kukiuka Taratibu Za Kazi08 Sep 20160
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameiagiza Sekretarieti ya M...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment