March 15, 2025 02:22:00 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Jeshi la Polisi Kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Dar es Salaam limekusanya shilingi milioni 320.2 ambapo fedha hizo ni kutokana na tozo za makosa ya usalama barabarani.

Askari wa kikosi cha usalama barabarani Jijini Dar es salaam akiwa kazini.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Kamanda wa wa polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Simon Sirro amesema fedha hizo ni kutokana na makosa 10,676 ambayo yamefanywa na watumiaji wa vyombo vya moto.

‘’Toka tarehe 25 hadi tarehe 28 tumefanikiwa kukusanya kiasi nilichotaja ambapo makosa mengi ya madereva wa bodaboda tumeanza kuona kwamb tunapowatoza faini ya elfu 30 au 60 haiwapi fundisho lolote ndiyo maana tumekuwa tumekuwa tukiwapeleka mahakamani ili kupunguza matukio ya uvunjifu wa sheria barabarani’’ Amesema Kamanda Sirro

Aidha Kamishna Sirro ametumia wasaa huo kuwataka watanzania kutii sheria bila shurti wanapokuwa wanatumia vyombo vya moto barabarani na katika maeneo yao ya kuishi.



Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
30 Jul 2016

Post a Comment

 
Top