Home
»
general news
» Raisi mstaafu,Jakaya Mrisho Kikwete Aingia Mtaani.....Afanya 'Shopping’ Mlimani City
Kwa mara ya kwanza tangu aondoke madarakani mwanzoni mwa mwezi huu, jana Rais Jakaya Kikwete alionekana akifanya manunuzi katika maduka yaliyopo jengo la Mlimani City, jijini Dar es Salaam.
Kikwete, ambaye alikuwa amevalia suti maarufu kama ‘kaunda suti’ yenye rangi nyeusi, alionekana akiingia katika viunga vya Mlimani City saa 5:00.
Mwandishi wetu ambaye alikuwepo katika viunga hivyo vya Mlimani Cityalishuhudia Kikwete akiwasili katika maeneo hayo akiwa katika msafara wa magari manne na pikipiki moja.
Rais huyo mstaafu pia alikuwa ameambatana na mkewe, Salma Kikwete, aliyekuwa amevalia mavazi ya kitenge pamoja na walinzi wao wanne.
Hatua hiyo ilionekana kushangaza baadhi ya watu waliokuwepo katika maeneo hayo, huku wengi wao wakionekana kutaka kumsalimia.
Mwandishi wetu ambaye muda wote alikuwa akimfuatilia Rais Kikwete na mke wake, alishuhudia wakiingia katika maduka ya Game na kufanya manunuzi kwa dakika zisizopungua 10 hadi 15 na baadaye kutoka nje na walinzi wake wakionekana kubeba mifuko iliyokuwa na bidhaa walizonunua.
Kama ilivyo hulka ya Rais Kikwete alipotoka nje ya duka hilo alianza kusalimiana na mtu mmoja ambaye alionekana kufahamiana naye.
Hatua hiyo ilimpa fursa ya kuwasalimia watu wengine waliokuwa karibu na tawi la benki moja.
Baada ya hapo msafara wake uliondoka na kuelekea Barabara ya Sam Nujoma.
Tangu achaguliwe kuwa rais mwaka 2005 itifaki na majukumu yake ya urais yalikuwa yakimbana Rais Kikwete na hivyo kushindwa mambo yake binafsi kama walivyo raia wengine.
Pamoja na kwamba Kikwete sasa ni raia, lakini kutokana na wadhifa aliowahi kuushika wa urais bado halingani na raia wengine wa kawaida, ingawaje majukumu ya urais yamepungua na hivyo kumpa fursa ya kutembea katika maeneo ya wazi na kufanya matumizi ya kawaida kama alivyofanya jana.
Tangu alipoachia kiti cha urais na kumkabidhi Dk. John Magufuli baada ya kuapishwa Novemba 5, Kikwete amekuwa akiishi nyumbani kwake Msoga, mkoani Pwani.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Jamaa Aliyejitosa Zoo Aliwe na Simba Laivu Alikuwa Anadai Mwisho wa Dunia Umefika...23 May 20160
Inasikitisha kwakweli, ameokolewa.... na simba walioanza kumla waliuwawa. aliingia kwenye jumba ...Read more ?
- Watumishi HEWA Waziponza Benki.......Benki za Dar es Salaam Zalimwa Barua Kurejesha Mamilioni ya Shilingi23 May 20160
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametoa siku 21 kwa benki zilizokuwa zikitumika kuwek...Read more ?
- Waziri Nchemba Afanya Ziara Ya Kushtukiza Saa Saba Usiku Machinjio Ya Ukonga Mazizi Na Kufukuza Viongozi Wote Wa Machinjio12 Feb 20160
Waziri wa Kilimo na Mifugo Mwigulu Nchemba amefanya ziara ya Kushtukiza saa saba usiku...Read more ?
- Askofu Gwajima, Sheikh Wa Mkoa Dar Wakwama Kumjulia Hali Mufti12 Feb 20160
Jopo la Madaktari wanaomtibu Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Abubakar Zubeir wamezuia ...Read more ?
- Siku 100 za Rais Magufuli: Hospitali Ya Muhimbili Yang'aa, Mapato Yapaa na Upatikanaji wa Dawa Waongezeka Kwa Asilimi 9611 Feb 20160
HOSPITALI ya Taifa ya Muhimbili (MNH) iliyopo jijini Dar es Salaam imesema ndani ya siku 100 z...Read more ?
- Lowassa Atakiwa Kuvisaidia Vyombo Vya Dola Kukabiliana na Tishio La Kundi la al Qaeda Kuingia Nchini10 Feb 20160
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed amemtaka Wa...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment