Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Ray na Johari Katika Pozi
SIKU chache baada ya kupenyezwa kwa madai ya kupata bwana mpya, staa wa filamu Bongo, Blandina William Chagula ‘Johari’ ameibuka na kuweka wazi kuwa kamwe hafikirii wala hana mpango wa kuachana na msanii mwenzake, Vincent Kigosi ‘Ray’ katika masuala ya kazi.

Akianika mwanya’ na Risasi Jumamosi hivi karibuni ndani ya ofisi zake, Sinza-Mori jijini Dar, Johari alisema hawezi kuruhusu mapenzi yatawale maisha yake na kusahau kazi.

“Siondoki RJ, kama kuna mtu anatarajia nitoke hapa eti kisa mambo ya mapenzi, anajidanganya kabisa, sifikirii kuachana na Ray kikazi, ni mtu muhimu sana, mapenzi hayawezi kutawala maisha yangu, yeye atabaki na mpenzi wake na mimi nitaendelea na mpenzi wangu,” alisema Johari.

Ray kwa sasa ameshaonesha upande na kukiri kukolea kwenye penzi la mwigizaji  Chuchu Hans na tayari ameshajipambanua kuwa wana mipango endelevu maishani mwao.

Chanzo: GPL

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top