Kama uko karibu na stori za TZ najua hautakuwa umesahau kuhusu ishu ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi βSuguβ na mzazi mwenzake, Faiza Ally.. Mbunge huyo hakuridhishwa na mavazi ambayo mzazi mwenzake alionekana nayo sehemu mbalimbali akaipeleka ishu Mahakamani kwamba kutokana na mama wa mtoto anavyoonekana yeye haridhishwi mtoto kuendelea kulelewa na Faiza.

Chanzo cha yote ilikuwa ni aina ya mavazi, leo kwenye show ya #Nirvana @EATV Faizaalikuwa kwenye Interview na ishu kubwa ilikuwa kuhusu mavazi yake >>>>βNapenda kuvaa vitu ninavyovaa, sina mavazi special naweza kuvaa vyovyote, niliipenda idea ya kuvaa nepi (diapers) na sina tatizo nayo kabisaβ

Faiza ni mama wa mtoto mmoja wa kike, kwenye upande wa malezi ikoje? >>> βMimi ni mama mzuri sana, ninamtazama mtoto wangu saa 24β¦ mavazi yangu hayaingiliani kabisa na malezi ya mtoto wanguβ¦ namlea kwa mazingira ya heshima, heshima na nguo ni vitu tofautiβ¦ ninavaa mavazi ninayopenda na bado nina heshima kwa watu. Sio lazima kila mtu akubali ninachofanya, ninapofanya kitu kwa watu kukubali au kukataa ni matatizo yaoβ >>> Faiza Ally.

Kuna kitu chochote anachojutia kutokana na mavazi yake? >>> βSina ninachojuta, niko sawaβ¦ tukio ambalo sijafurahia ni moja la kupelekwa Mahakamani na kunyangβanywa mtoto wangu kitu ambacho ninakifanyia kazi na kinaenda vizuri.. sioni tukio baya zaidi ya watu kunitukana na ni kawaidaβ¦ ninaenjoy na ninapenda mavazi yanguβ >>>>

Haya ndio maneno yake kuhusu nguo aliyoivaa kwenye KTMA 2015 >>> βIdea ilikuwa ni nzuri mpaka pale ambapo nguo iliachanaβ¦ lengo lilikuwa sio kuacha makalio wazi, ile nguo baada ya kukaa kwenye gari ilishuka na sehemu ya makalio ikabaki waziβ¦ Wakati natoka nyumbani ilikuwa imekaa tu vizuri, nilivyoshuka kwenye gari sikujiangalia, nilipofika red carpet nikapigwa pichaβ >>>>

Anatoka kwenye familia inayofuata Dini? >>> βBaba yangu sijawahi kumwona anakwenda Msikitini, sio kwamba naikana dini lakini sijazaliwa kwenye familia ya kidini.. maisha yangu yako hivi miaka yote na hakuna kilichobadilika kwenye maisha yanguβ¦ nafurahia maisha yanguβ >>>>
Huu ndio ushauri wake kwa wasichana kuhusu ishu ya fashion za mavazi >>>> βWasichana wajue kwamba kilicholeta gumzo ilikuwa bahati mbaya, ila wawe huru wavae vitu wanavyovifurahia ila isitokee kama ileβ¦ kuna mavazi navaa na kuna mavazi siwezi kuvaaβ >>>>

Matukio ya mavazi yake yamempa umaarufu? Amepanga kufanya chochote? >>>> βSijapanga chochote, sikujua kama itakuwa ni umaarufuβ¦ mimi ni mwigizaji na ninaandika kitabu, labda kwa kazi zangu hizoβ¦ kipande kilichoonekana sio maisha yangu yote, ni sehemu ya mwiliβ¦ Faiza ni mwanamke mzuri, anayejielewa, mwenye akili timamu, mama bora, anayejipenda, mtu wa watuβ >>>> Faiza Ally.

Kwenye Interview hiyo alikuwepo pia mwanamitindo Ally Rehmtullah, haya ndio maneno yake kuhusu nguo ya Faiza >>>> βUbunifu wake ulikuwa mzuri labda mawasiliano kati ya yeye na mbunifu wake hayakuwa mazuri, vazi kama lile kwa utamaduni wetu lazima watu watashtuka watakusema, ni muhimu kujua yeye mwenyewe Faiza alikuwa anataka niniβ¦ Naamini ilikuwa bahati mbaya, ingekuwa ni mimi ile gauni nisingevaaβ >>>> Ally Rehmtullah.
Majibu ya Faiza Ally yako pia kwenye hii sauti niliyorekodi kipande cha Nirvana mtu wangu, unaweza kuplay kumsikiliza mwenyewe
SOURCE:Millard Ayo
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment