March 19, 2025 06:42:37 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Screen-Shot-2015-06-28-at-10.19.33
Wakati huu mashabiki wa Arsenal wakisubiri golikipa wa Chelsea, Petr Cech kujiunga Emirates, kuna taarifa mpya kwamba kiungo wa Chile na Juventus, Arturo Vidal naye yuko mbioni kutua Kaskazini mwa London.
Vidal ambaye anaitumikia Chile katika michuano ya Copa America inayoendelea katika ardhi yao,  kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa kutua England hususani katika klabu ya Manchester United.
Leo tetesi zimeibuka kwamba Vidal ataondoka Juventus majira haya ya kiangazi na tayari amekubali dili la kujiunga na Arsenal ambalo litatangazwa baada ya Copa America kufikia tamati.
Tetesi hizo zimeibuka saa chache zilizopita kutoka kwa Mwandishi wa habari wa Chile, Hernan Feler ambayo amethibitisha kwenye radio kwamba Arsenal wamemsajili Vidal.
Feler ni chanzo makini cha habari? bado haijulikani, lakini idadi kubwa ya mashabiki wa Arsenal wanadai ndiye alikuwa wa kwanza kutangaza taarifa za Alexis Sanchez kutua Arsenal kutokea Barcelona.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
29 Jun 2015

Post a Comment

 
Top