Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

MWILI wa  Mufti ,Alhaj Sheikh Shaban Issa Bin Simba unataraji kusafirishwa leo Jumanne Juni 16 saa 3 asubuhi, kuelekea mkoani Shinyanga kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata), Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaj  Mussa Salum, amesema mwili wa marehemu utaswaliwa kesho (leo) katika Msikiti wa Msilimu, viongozi mbalimbali wa dini na serikali watakuwepo.

Amesema marehemu amefikwa na umauti huo, baada ya kusumbuliwa sana na sukari,Shinikizo la Damu (BP)  pamoja na Figo.

Hata hivyo amesema kuwa juzi (Jumapili) Mufti alifanyiwa oparesheni ya figo katika Hospitali ya TMJ Jijini Dar es Salaam.

Salum amesema marehem anatarajiwa kuzikwa leo jumanne majira ya saa kumi arlasiri mkoani mkoani Shinyanga .

 Sehemu ya wanawake waliofika nyumbani kwa Marehemu  Mufti Alhaj Sheikh Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B jijini Dar es Salaam .
Sheikh Mkoa wa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akibadilishana mawazo na Sheikh wa Mkoa wa Kigoma Hassan Kiburwa walipofika nyumbani kwa Marehemu Mufti ,Mikocheni B  jijini Dar es Salaam
Kulia ni Sheikh wa Mkowa Dar es Salaam,Alhaj Sheikh Alhad Mussa Salum akiwa na baadhi ya Masheikh waliofika Nyumbani kwa Marehen Mufti,Shabaan Issa Bin Simba Mikocheni B Jijini Dar es Salaam.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top