March 16, 2025 04:41:59 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MWANADADA anayefanya vizuri kwenye tasnia ya filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ ameibuka na kusema hawezi kumrudia aliyekuwa mpenzi wake, msanii Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’.
Akizungumza na gazeti hili mwishoni mwa wiki, Nisha alisema amelazimika kutoa ufafanuzi huo baada ya kuenea kwa uvumi kuwa ana mpango wa kurudiana naye, jambo alilosema haliwezekani kwani kwake hana tabia ya kula matapishi.
“Siwezi kurudiana na Nay,  kwanza ana mwanamke mwingine na kuzaa naye japo wameachana, mwanzo nilimuogopa sana nikimuona, lakini hivi sasa nimeshamzoea, tumebaki kama kaka na dada, suala la mapenzi haliwezi kujirudia tena,” alisema.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
17 Jun 2015

Post a Comment

 
Top