March 17, 2025 10:06:36 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza amesogeza mbele uchaguzi wa wabunge kwa siku 10 hadi Juni 5 mwaka huu kufuatia jaribio la mapinduzi.

Msemaji wa Rais, Willy Nyamitwe ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa kufuatia jaribio la mapinduzi la wiki iliyopita na vurugu zilizofuatia ni bora kusogeza mbele uchaguzi huo kwa muda.
 
"Uchaguzi huo wa wabunge ulikuwa umeratibiwa kufanyika Mei 26 mwaka huu lakini sasa inatubidi kuusogeza mbele mpaka Juni 5 mwaka huu ili kuwasikiza washirika wetu wa kimataifa pamoja na tume ya uchaguzi ambayo pia inatumia muda huo kutatua maswali yaliyoulizwa na vyama vya upinzani" alisema Nyamitwe.

Mpaka sasa tarehe rasmi ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanywa Juni 26 mwaka huu bado haijabadilika na nia ya Rais Nkurunziza kuwania urais kwa muhula wa tatu ipo palepale.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
20 May 2015

Post a Comment

 
Top