Home
»
Matukio
» Ukistaajabu ya Musa Utayaona ya Firauni...Kaburi Lafukuliwa Wamvua Maiti Suti, Soksi na Viatu Kisha Kutokomea Navyo
Kaburi likiwa wazi baada ya kufukuliwa.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linawasaka watu wanaosadikiwa kuwa ni wezi ambao wamebomoa kaburi la marehemu Napegwa Kishaluli (75), mkazi wa Mailimoja Kibaha na kuutoa mwili wake kisha kuiba suti, viatu na soksi alizokuwa amevalishwa.
Habari za kipolisi kutoka mkoani Pwani zinasema kuwa, marehemu alizikwa Aprili 20, mwaka huu lakini siku saba baadaye watu wasiojulikana walikwenda kaburuni na kulivunja kisha kulitoa jeneza wakidhani kulikuwa na mali kaburini kisha kumvua nguo zote marehemu wakidhani alikuwa na dhahabu.
Tukio hilo lilitokea Aprili 24, mwaka huu katika Kata ya Tangini jirani na Soko la Loliondo, habari zinasema baada ya mazishi kaburi hilo liliwekewa mlinzi kwa muda wa wiki moja kutokana na uvumi kuenea kuwa marehemu alizikwa na vitu vya thamani ukiwemo mkufu wa dhahabu.
Watu wa karibu na familia ya marehemu wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo na wakasema kuwa baada ya mazishi ulikuwepo uvumi kwamba marehemu alizikwa na vitu vya thamani kama vile pete na mkufu wa dhahabu, kitu ambacho siyo kweli.
Akizungumza na mwandishi wetu, ndugu wa marehemu ambaye hakutaka jina lake kuandikwa gazetini kwa kuwa siyo msemaji wa familia, alisema baada kuzika walilazimika kuajiri mtu wa kulinda kaburi hilo la ndugu yao kwa wiki moja lakini siku moja baada ya mkataba kumalizika kaburi hilo lilivunjwa.
“Tuliweka mlinzi alinde kaburi hilo kwa wiki moja tukiamini litakuwa limekauka kwa sababu lilitengenezwa kwa zege. Tuliamini watu wenye nia mbaya watashindwa kulivunja jambo ambalo limekuwa kinyume kwa vile baada ya muda huo kumalizika kaburi lilibomolewa ‘ubavuni’ na watu wasiojulikana ambao waliamini ndani ya kaburi kulikuwa na mali nyingi,” alisema.
Aliongeza kuwa baada ya kuvunja kaburi hilo wahalifu hao walilitoa jeneza nje, wakalifungua kisha kupekua ndani kwa kuligeuza na kuliweka tofauti na lilivyokuwa awali.Baada ya kuona hakukuwa na mali zozote waliamua kumvua marehemu nguo zote, viatu na soksi alizovalishwa wakaondoka nazo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, ACP Jafari Mohamedi juzi alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na akaongeza kwamba watu hao hawajakamatwa.“Bado tupo kwenye uchunguzi na watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria,” alisema.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment