Home
»
Entertainment
» Majibu ya DNA Test Aliyoifanya NAY WA MITEGO Kubaini Kama Mtoto Aliyezaa na SIWEMA ni Wake Ama Laa Yametoka..Majibu Haya Hapa
Baada ya utata mzito kutawala kwenye vyombo vya habari juu ya uhalali wa mtoto wa Mbongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ kwa mzazi mwenzake Siwema Edson, hatimaye kipimo cha vinasaba (DNA) kimetoka na kumaliza ubishi kwamba mtoto huyo aitwaye Curtis ni damu halisi ya msanii huyo.
Hivi karibuni, Nay na Siwema ambao walikuwa wapenzi kisha kumwagana, waligombana na kila mmoja kuzungumza lake juu ya mtoto wao huyo ambapo Siwema alidai si damu ya Nay wakati msanii huyo alisema ni damu yake.
Licha ya kupokea majibu hayo mazuri kwake, Nay aliyachukua majibu hayo kwa kuangua kilio cha furaha huku akieleza ya moyoni kuhusiana na sakata hilo.
“Hili ni swala ambalo lilikuwa linaniumiza kichwa kila kukicha. Unajua kama mwanaume, mtu akwambie mtoto si wako unadhani ni maumivu kiasi gani utayapata? Inauma sana, mtu umelea kuanzia mimba hadi mtoto amezaliwa, si kitu kidogo.
“Namshukuru Mungu kwa majibu kwamba ni damu yangu. Mashabiki wangu watambue tu kwamba, Curtis ni mwanangu asilimia mia hivyo hakuna ubishi tena.
“Ujue nampenda sana mwanangu na kwa bahati nzuri huyo ndiye mwanangu wa kiume pekee, hivyo sikutaka kuruhusu wazo lolote kutoka kwa mtu mwingine maana hata kama majibu yasingesema kama ni wangu nilikuwa radhi kuishi naye na kumlea bila kujali hilo kwa sababu tu niliamini siku zote ni mali yangu,” alisema Nay.
Nay aliingia kwenye utata huo takriban mwezi mmoja uliopita baada ya kupishana kauli na Siwema ambaye alimfumania akiwa na mwanaume mwingine nyumbani kwake, jijini Mwanza na kuamua kumchukua mtoto kisha kuishi naye jijini Dar kwa msaada wa mama yake mzazi.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Diamond kuwania tuzo 5 za Afrima 2016, Alikiba na Yamoto Band moja08 Sep 20160
Diamond Platnumz ametajwa kuwania vipengele vitano kwenye tuzo za mwaka huu za Afrima. Vipeng...Read more ?
- Ujumbe wa Diamond kwa bintiye Wazua Gumzo......Kamwambia "Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana"23 Jul 20160
Diamond Platnumz si mgeni kwenye jumbe tata kwenye mitandao ya kijamii. Lakini ujumbe wake mpya...Read more ?
- Bifu Kali Kati ya Diamond na Clouds Media23 May 20160
Ni dhahiri sasa msanii wa kimataifa Diamond na brand kubwa ya radio na tv Clouds Fm, bifu la hadh...Read more ?
- Afande Sele Aungana Na Mbunge Joseph Msukuma Kuitaka Serikali Ihalalishe Matumizi Ya Bhangi02 Feb 20160
Msanii mkongwe wa hip hop nchini, Afande Sele amefunguka na kusema serikali ihalalishe matumiz...Read more ?
- Gari Jipya Analomiliki Masanja Mkandamizaji.10 Jan 20160
Msanii wa Vichekesho Anawakilisha kundi la Orijino Komedi anayejulikana kama Masanja Mkand...Read more ?
- Zari The Lady Boss Awakosha Mashabiki wa Penzi lake na Diamond Kwa Picha Hizi09 Jan 20160
Zari the Boss Lady ‘Mama Tiffah’ amewakosha mashabiki wa penzi lake na Diamond ‘Baba Tiffah’ baada...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment