March 15, 2025 01:12:00 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Katika gazeti la changamoto katika ukurasa wake wa kwanza unasomeka "Zitto azidi kuwaumiza CHADEMA" na habari hiyo ukiifuatilia ndani inaeleza kuhusu kauli ya mwenyekiti wa CHADEMA, mhe Mbowe na jinsi Zitto alivyoipokea.


Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kwamba, Zitto hakutarajia mtu ambae yeye anamuheshimu katika siasa kuwa na misimamo isiyo tanguliza maslahi ya taifa mbele na badala yake kushikilia matatizo yao yaliyojitokeza huko nyuma ambayo kimsingi yalihusu nafasi za kiuongozi.

Zitto alieleza kuwa kwa sasa hayupo tayari kujibizana na viongozi tena kwa kuwa amekuwa akisema hivyo kila mahali anapokwenda kufanya mikutano yake na amewekeza nguvu nyingi katika kukitangaza chama chake kipya. Pamoja na malengo hayo, ila kwa kauli ile ya jana ameona hana budi kuitolea maelezo!

Zitto alisisitiza kuwa matatizo yake binafsi na viongozi wa chama chake cha zamani yasipewe kipaumbele kuliko maslahi ya taifa. Ameeleza kuwa mara kadhaa ameomba chama chake kijiunge na UKAWA lakini CHADEMA wamekuwa wakigoma. Kauli ile ya jana sio ngeni masikioni pangu. Alieleza Zitto.

Zitto aliongezea kuwa, "kama ni matatizo basi ni kati yangu na viongozi wa CHADEMA na yasifanywe ya taifa zima. ACT-Wazalendo tuna nia ya dhati ya kuwaondoa CCM madarakani. Pia UKAWA wana nia hiyo hiyo. Kwa hali hiyo hatuna budi kushirikiana kummaliza CCM na hilo litafanyika kama kweli tumetanguliza utaifa mbele badala ya matatizo yetu binafsi na viongozi wa chama changu cha zamani."

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
28 Apr 2015

Post a Comment

 
Top