Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Msanii mkubwa Bongo Hamis Baba Maarifu Kama H Baba kwenye Music Amemuandikia Waraka wa kumpa hongera mke wake Frora Mvungi baada ya kumshuhudia laivu akijifungua mtoto wa Pili hospitalini..

Flora amejifungua mtoto wa pili ambae amepewa jina la Afrika huku H baba akishihudia jinsi mkewe huyo aliyokuwa anamleta Africa Duniani.

"Huyu ni mtoto wa pili mke wangu anajifungua nashuhudia mwanzo wa uchungu mpaka kujifungua kwake kwa kweli heshima kubwa kwa mama Tanzanite ulijitahidi sana nakupa hongera kwa kweli wewe ni shujaaa na ni mfano wa kuigwa" ulisomeka waraka huo

Waraka huo uliendelea kusema:

"Kuna muda nilikuwa navumilia na kutamani kutoka nje ili nisione unavyojifungua lakini nilijikaza na kuangalia mpaka mwisho wake Asante mungu kwa watoto hawa wawili mungu awajalie wakue vizuri"

Hongera Sana H-baba na Flora Mvungi

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
27 Apr 2015

Post a Comment

 
Top