DHAMBI? Neema Pangani, mkazi wa jijini Dar alijikuta akiangua kilio kanisani wakati mumewe Daniel Mhina alipokuwa anamuoa mke wa pili, Irene Lema, Risasi Mchanganyiko lina stori kamili.
Tukio hilo lilitokea Jumapili iliyopita katika Kanisa la Evangelistic Assemblies of God (EAGT) Bonde la Baraka lililopo maeneo ya Alimaua Kijitonyama jijini Dar, ambapo Mchungaji Kiongozi Asheri Mwaisunga ndiye aliyebariki ndoa hiyo.
Wakati ndoa inafungwa katika kanisa hilo, mke halali wa Daniel, Neema ambaye naye ni muumini wa kanisa hilo, aliamua kutoka nje na kuangua kilio. “Ndoa yangu na Daniel tulifunga Desemba 15, mwaka 1991 katika Kanisa la Evangelistic Assembies of God Tanzania (EAGT), Uzuri Manzese jijini Dar ambapo mchungaji Asheri Mwaisunga (huyohuyo aliyefungisha ya pili) ndiye aliyefungisha ndoa hiyo.
“Wakati naposwa na mume wangu Daniel nilikuwa tayari nina mtoto ambaye nilikuwa nimezaa na mwanaume mwingine lakini nikasikia kuna mama alikuwa anataka Daniel amuoe ndugu yake, nikamuuliza mume wangu akasema hapendi kupangiwa mtu wa kumuoa kwa sababu ndoa ni ya watu wawili na mimi ndiye nilikuwa chaguo lake,” alisema Neema na kuzidi kumwaga maelezo kuwa, mchungaji huyo aliposikia matatizo yao, alimshauri Daniel atafute mwanamke mwingine akidai yeye hana kizazi.
Kwa upande wake Daniel, alijitetea kuwa yeye amefunga ndoa ya bomani Ijumaa iliyopita na pale kanisani alikuwa akibariki na amefanya hivyo baada ya kugundua mke wake ana matatizo.
“Ni kweli nimefunga ndoa lakini ni ya bomani na nilitoa tangazo siku 21 kabla, hakukuwa na kipingamizi chochote na pale kanisani juzi nilikuwa ninabariki ili nipate baraka kutoka kwa mchungaji wangu ambaye nilimuomba baada ya kuona kwamba mimi ni muumini mzuri,” alisema na kusisitiza mkewe huyo wa zamani alikuwa na matatizo.
Mchungaji Asheri Mwaisunga alipotafutwa kwa njia ya simu alijitetea na kudai kuwa yeye hakufungisha ndoa hiyo ila alikuwa akiibariki baada ya kufungwa bomani: “Mimi sikufungisha hiyo ndoa kwani tayari walishafungishwa na Mkuu wa Wilaya na baada ya pale ndiyo wakaja kanisani kwa ajili ya kubarikiwa, mkitaka vielelezo kamili kuhusu hilo nendeni kule mtapata.”
Hata hivyo gazeti hili lilinasa picha za Daniel akionekana kusaini cheti cha ndoa kanisani hapo licha ya mchungaji na Daniel kudai pale walikwenda kubariki.
>>>>>GPL
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- BREAKING NEWS: Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza rasmi tarehe ya kurudiwa kwa uchaguzi mkuu wa Zanzibar22 Jan 20160
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Jecha Salim Jecha ametangaza rasmi tarehe ya kuru...Read more ?
- Rais Dkt. Magufuli Amteua Jakaya Kikwete Kuwa Mkuu Wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam.21 Jan 20160
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Rais Mstaafu wa awamu ...Read more ?
- JANUARY MAKAMBAASHANGAZWA NA HAYA MAGAZETI MATATU KUHUSU LOWASSA02 Sep 20150
Naibu waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba ameonesha kushangazwa na mfa...Read more ?
- Polisi Yakamata Majambazi 38 Yakiwa na silaha Nzito pamoja na Milioni 170......Majambazi hayo yanadaiwa na mafunzo ya Kijeshi01 Sep 20150
Jeshi la Polisi limewakamata watu 38 wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi ambao pia wamepatiwa mafun...Read more ?
- Wananchi Wafunga Barabara Baada ya Gari la Polisi Kugonga Wanafunzi wawili31 Aug 20150
Wananchi wa eneo la Misugusugu Wilayani Kibaha Mkoani Pwani hii leo wamefunga barabara baada ya...Read more ?
- Hali Tete Bunda, Viongozi CHADEMA Wajiuzulu...Kisa Ester Bulaya22 Aug 20150
SIKU chache baada ya mgombea ubunge wa Jimbo la Bunda Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maend...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment