Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Dr.Reginald Mengi na Bukhary Kibonajoro
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr.Reginald Mengi amesema Watanzania wanaweza kuondokana na umaskini iwapo mawazo na fikra sahihi zitatumika kuwawezesha wananchi wake kutumia rasilimali za asili kujikwamua kiuchumi. 
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dr.Reginald Mengi ameyasema hayo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya kuwatangaza na kuwazawadia washindi wa mwezi wa Marchi wa shindano la Tweet wazo la biashara alilolianzisha ili kuwahamasisha watanzania kujikomboa kiuchumi.

Mshindi wa kwanza kwa mwezi Marchi aliyezawadiwa ruzuku ya shilingi milioni 10 ni mhitimu wa elimu ya Kompyuta wa  Chuo Kikuu cha Dar es salaam  Bukhary Kibonajoro, aliyebuni wazo la kutengeneza Program ya kompyuta ya kusimamia biashara za wafanyabiashara wadogo.

Washindi wengine 9 ambao mawazo yao yaliingia katika 10 bora walizawadiwa shilingi milioni moja kila mmoja.Hao ni pamoja na Salim Said, Harry Kageyo,Abdallah Mdira,Victor Byemelwa, na  Norman Billy.Wengine ni Atumilikye IsaacStephen Maswe, Irene Enock na Joyce Patrick Tano.

Mapema Mkuu wa jopo la majaji Dr. Donath Ulomi, na Jaji mwenzake Dr.Jabu  Mwasha walisema mwezi uliopita idadi ya Twitter zilizopokelewa na kushindanishwa zilikuwa ni nyingi kuliko miezi iliyopita,na kutoa ushauri wa namna bora ya kubuni wazo bora.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top