Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This


Star wa bongo flava anayeiwakilisha kanda ya ziwa, Hussein Machozi yuko kwenye mazoezi makali ya kujiweka sawa kwa ajili ya kukipiga na moja kati ya timu inayoshiriki ligi kuu bara msimu ujao.
Akizungumza kupitia kipindi cha “Hatua tatu” ya Times fm, Hussein amedai msimu ujao atasakata gozi kwenye ligi kuu bara na timu ya Kagera sugar.
“Nipo mazoezini sasa hivi kwa ajili ya kujiandaa na kusajiliwa na Kagera Sugar kwa ajili ya kuichezea msimu ujao, so mazoezi wanakuja wananitazama kila siku, kwa hiyo mashabiki watambue msimu ujao wataniona kupitia soka” alisanua Machozi.
Katika line nyingine amesema ilikuwa aichezee muda mrefu Kagera Sugar, lakini hakukuwa na maelewano mazuri kati yake na kocha wa walima sukari hao.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
29 Apr 2015

Post a Comment

 
Top