Home
»
Entertainment
» Kuhusu zilizosambaa juu ya kifo cha Hussein Machozi, makubwa mengine yametokea nyumbani kwao Singida.
Ni jioni ya Jumatano ya April 15 2015 nipo ofisini na naanza kupokea simu nyingi za watu wangu wakitaka kujua ukweli kuhusu taarifa zilizoenea kwamba msanii wa bongofleva Hussein Machozi amefariki kwenye ajali iliyohusisha gari la mizigo na gari dogo Dodoma.
Baada ya hapo naanza kupiga simu ya Hussei Machozi inaita lakini haipokelewi kwa zaidi ya nusu saa, naanza kupata wasiwasi, nikiwatafuta rafiki zake pia sifanikiwi lakini baadae naendelea kuipiga simu ya Hussein na inapokelewa.
Sauti ni ya Hussein mwenyewe, anaanza kwa kusema ‘Nilijiandaa hapa nimekwenda mazoezini kucheza mpira, niliacha simu yangu kwenye charge na niliporudi baada ya mazoezi nakuta missedcalls nyingi sana, msg na simu za mama yangu pamoja na dada, wakati najiandaa kuanza kupiga simu ghafla naanza kupata simu za watu mbalimbali kwamba nimepata ajali na kufariki, mimi nikawaambia sio kweli mimi ni mzima na nipoDar es salaam‘
Kumbe baada ya taarifa za kifo kusambaa na kuwafikia Mama yake mzazi pamoja na dada yake ambao walipiga simu yake na haikupokelewa kwa muda mrefu, wakaamini kweli kilichotokea ni kifo…. mama akazimia hapohapo, dada akaanguka na kuzimia vilevile.
Sasa hivi Hussein inabidi alazimike kusafiri mpaka kwao Singida Manyoni ili kuwahakikishia ndugu zake kwamba yuko hai manake aliongea kwenye simu ya kaka yake na kumpa Dada simu baada ya kuzinduka lakini dada hajaamini, kasema anafichwa tu lakini ni kweli Hussein kafariki.
Mama anaendeleaje? ni yapi mengine ameyasema Hussein Machozi? bonyeza play hapa chini kumsikia mwenyewe…CREDIT: Millardayo
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Diamond kuwania tuzo 5 za Afrima 2016, Alikiba na Yamoto Band moja08 Sep 20160
Diamond Platnumz ametajwa kuwania vipengele vitano kwenye tuzo za mwaka huu za Afrima. Vipeng...Read more ?
- Ujumbe wa Diamond kwa bintiye Wazua Gumzo......Kamwambia "Ukikua chonde mama ukitunze wasikile sana"23 Jul 20160
Diamond Platnumz si mgeni kwenye jumbe tata kwenye mitandao ya kijamii. Lakini ujumbe wake mpya...Read more ?
- Bifu Kali Kati ya Diamond na Clouds Media23 May 20160
Ni dhahiri sasa msanii wa kimataifa Diamond na brand kubwa ya radio na tv Clouds Fm, bifu la hadh...Read more ?
- Afande Sele Aungana Na Mbunge Joseph Msukuma Kuitaka Serikali Ihalalishe Matumizi Ya Bhangi02 Feb 20160
Msanii mkongwe wa hip hop nchini, Afande Sele amefunguka na kusema serikali ihalalishe matumiz...Read more ?
- Gari Jipya Analomiliki Masanja Mkandamizaji.10 Jan 20160
Msanii wa Vichekesho Anawakilisha kundi la Orijino Komedi anayejulikana kama Masanja Mkand...Read more ?
- Zari The Lady Boss Awakosha Mashabiki wa Penzi lake na Diamond Kwa Picha Hizi09 Jan 20160
Zari the Boss Lady ‘Mama Tiffah’ amewakosha mashabiki wa penzi lake na Diamond ‘Baba Tiffah’ baada...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment