Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
family
Huwa inatokea Mwanaume anataka kumuoa mrembo flani lakini wazazi wa Mke mtarajiwa wanakataa mtoto wao kuolewa na jamaa labda kwa sababu za kidini, kitabia au kitabaka.

Basi hii imetokea Pakistani ambako Gul Ahmed Said amemuua Baba Mkwe mtarajiwa pamoja na watu wengine tisa wa familia yake baada ya kukataliwa kumuoa Binti wa Mzee huyo huko Charsadda.
Pakistan
Charsadda
Binti aliekua anataka kumuoa ni binamu yake ambapo Polisi wa Pakistani wamesema ugomvi ulianzia kwenye mabishano ya idadi ya dhahabu kwenye harusi.
Waliouwawa kwa risasi ni Watoto nane wa mzee huyo, mzee mwenyewe pamoja na mke wake ambapo Polisi bado wanaendelea kumtafuta Said ambaye amekua akitafutwa kutokana na mauaji mengine aliyoyafanya November 2014 kwa kuwaua Wazazi wake, kaka yake pamoja na shemeji yake.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top