Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Treni ambayo ilikuwa na kichwa kimoja ikielekea kuchukua mabehewa asubuhi ya leo imegongwa na gari kubwa la mizigo eneo la Karume jijini Dar na kusababisha foleni ndefu eneo hilo.
 
Tukio hilo limejiri asubuhi ya saa 12 alfajiri ambapo gari hilo lilikuwa likipita kwa kasi bila kufuata alama za barabarani zinazoonesha sehemu ya reli.
 
Akizungumza na mwandishi wetu, Ofisa Oparesheni Shirika la Reli, Mohamed  Kanka,  alisema kuwa treni hiyo ilikuwa ikipita majira ya saa kumi na mbili alfajiri na kugongwa na gari iliyokuwa ikipita pasipo dereva wa gari hiyo kuzingatia alama iliyokuwa ikionesha kama sehemu hiyo kuna reli.
 
Alisema kuwa katika ajali hiyo dereva wa gari na dereva aliyekuwa katika treni hiyo wameumia na wamekimbizwa  Hospitali ya Amana Ilala kwa ajili ya kupatiwa matibabu.
 
Vilevile alisema baada ya ajali hiyo kutokea gari jingine lililokuwa limesimama liligongwa na kichwa cha treni baada ya kuiacha njia yake na kuelekea upande wa magari yaliyokuwa yakipita.
 
Ofisa huyo amewaasa madereva kuwa makini wanapofika eneo lenye alama kuonyesha mbele kuna reli kwani ajali nyingi hutokea kutokana  na madereva wasiokuwa waangalifu
Ulikuwa mshangao usiokwisha kwa watu kushuhudia kumbe treni linaweza kugongwa!
Gari lililogonga treni.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top