Msaniii wa Bongo fleva Nuh Mziwanda ambae ni mpenzi wa wa msanii Shilole amefunguka na kusema hakuna binadamu wa kuweza kuwatenganisha katika mapenzi yao licha ya manneo ya watu kuzungumza vibaya kuhusu mpenzi wake huyo ambae amekuwa akimpiga mara kwa mara.
Mziwanda alisema kuwa ni Mungu tu ndiyo anaweza kuwatenganisha na kama ni kipigo basi yeye amezoea maana hakuna mapenzi ya kweli bila kupigwa na kama hupigwi basi mpenzi wako hana wivu na wewe.
"Mungu ndio ataitenganisha hii couple.binadamu neeeeeeeeeeeever. Sawa ananibonda kila siku ila ndio tumependana wenyewe na kupigwa kuna raha yake jamani .Ukiona haupigwi ujue hakuna wivu hapo na mimi najua napompigia"
Lakini mbali na kupokea na kukubali hali ya maneno ya watu katika mitandao ya jamiii pia Nuh ameonyesha kutopenda kitendo hicho ambacho kimeonekana kurudiwa kama kiitikio cha wimbo mzuri
"Maana naona mmezidi sasa kila saa kipigo kipigo.Nisharidhika mimi bwege fala mjinga semeni yoooote ila ndo nishampenda na simuachi ng'o.Bora mfanye yenu tu na nawapenda saaaaaaana wanaofatilia mziki wangu"
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro








Post a Comment
Post a Comment