March 31, 2025 05:38:46 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
 
Habari za kusikitisha kutoka kijiji na kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ni kwamba watu zaidi ya 30 wanadaiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa nyumba kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo.

Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa mvua kubwa iliyoambatana na upepo,mawe imenyesha usiku wa kuamkia leo na kuangusha nyumba na miti katika eneo hilo.

Hali hiyo inadaiwa kuleta majanga zaidi kutoka na nyumba zilizojengwa kwa udongo kuharibiwa vibaya na mvua hiyo kubwa.

Habari kutoka eneo la tukio zinasema hali siyo shwari kwani nyumba nyingi zimeharibiwa vibaya,miti imeanguka na sasa miili ya marehemu na majeruhi inakimbizwa katika hospitali ya Kahama.
Malunde1 blog imeambiwa kuwa hadi sasa mvua bado inaendelea kunyesha ingawa siyo kubwa kama ile ya usiku na viongozi mbalimbali wa serikali kutoka wilayani Kahama wamefika eneo la tukio.


kibonajoro.com inafuatilia tukio hili,tutakuletea taarifa kamili hivi punde,endelea kutembelea kibonajoro.com

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
04 Mar 2015

Post a Comment

 
Top