March 13, 2025 08:02:44 PM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
Mwigizaji wa vichekesho wa Kundi la Orijino Komedi, Mujuni Sylivery aka Mpoki moja ya vitu ambavyo aliwahi kuvifanya katika kazi yake ya uchekeshaji ni pamoja na kuigiza sauti ya marehemu, Kapteni John KOMBA ambaye amefariki February 28.
Leo Mpoki amesikika kwenye Leo Tena CloudsFM, alianza kuzungumzia namna alivyopokea taarifa za msiba huo; “..Mtu akishatoweka kwenye ulimwengu akifariki dunia inauma kwa sababu mtu unayempoteza leo huwezi kumpata tena.. lakini ukimpoteza mbuzi utaenda Vingunguti utamnunua na sherehe itaendelea.. Kitendo cha kufariki mtu yoyote hata kama hajulikani ni pengo kubwa tu
Imeniathiri kwa kisanii kwa kuwa nilikuwa namuwezea, kidogo alikuwa hapendi lakini ilivyokuja akatulia.. Watu wakamwambia bwana hawa watoto tu.. Ukimuiga mtu ana mazuri huwezi kumuiga kwa mabaya tu.. ana mazuri yake..Ikanipa wigo mpana kwenye kazi yangu ya kubuni sauti yake, vitendo..
mwisho wa siku kaondoka pengo lake halitozibika.. Kama kuna la kufanya kuhusu yeye kwa kumuenzi sitokuwa nyuma, nitafanya ili mradi lisimvunjie heshima Marehemu, familia yake, jamii, viongozi wenzake Bungeni na watu wote ambao kawaacha kwenye jimbo lake sasa hivi wapweke..
Mpoki alikuwa akimuigiza marehemu Komba, na Komba hakuwa natatizo nae ila alimshauri awe anavaa na kuonekana mtannashati wakati anamuigiza kwani yeye (marehemu ) alikuwa ni mtanashati, Komba aliyasema hayo mwaka jana kwenye kipindi cha Mkasi.
Picha:Mpoki akiwa na baadhi ya waigizaji wenzake leo katika viwanja vya karimjee walipokuwa wakiuaga mwili wa Komba.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
03 Mar 2015

Post a Comment

 
Top