Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
preee
Tuliwahi kuandika stori ya mwanamke kujifungua watoto mapacha ambao walipishana miezi miwili waliozaliwa katika moja ya hospitali huko Romania na kuonekana kugusa hisia za watu wengi.
sarah3
Hii tena imetokea huko Uingereza baada ya mama mmoja kupata watoto wanne ikiwa ni matokeo ya kushika ujauzito mara mbili ndani ya mwaka mmoja.

Sarah Ward mwenye umri wa miaka 29 alipata mapacha watatu ikiwa ni mwezi mmoja tangu ajifungue mtoto wake wa kwanza wa kiume,
sarah
Mwanamke huyo alijifungua mapacha hao watatu ambao walizaliwa kabla ya muda huku mtoto wake wa kwanza akiwa tayari na miezi nane.
Sarah amesema anashukuru kupata watoto hao na amekua akitumia nepi zaidi ya 30 kwa siku kwa ajili ya kuwabadilisha watoto wake lakini haoni kama ni gharama kutokana na furaha aliyonayo.
sarah2
Alisema alipata wakati mgumu wakati akijaribu kushika mimba ya mtoto wake wa kwanza na madaktari walipogundua ana mimba ya watoto mapacha watatu walimshauri kumtoa mmoja ili watakaosalia waweze kukua vizuri lakini alikataa na kutaka waache wote.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top