Wasichana hawa wawili ni mapacha – japo hawaonekani kama hivyo.

Lucy, mwenye ngozi nyeupe, na nywele zilizonyooka za ginger na Maria mwenye nywele nene za curly na ngozi nyeusi, walizaliwa January 1997.

Unaweza kuamini warembo hawa ni mapacha? Lucy na Maria
Kutokana na tokeo nadra la kisayansi lililotokana na mama na baba yao waliochanganya rangi, walizaliwa wakiwa na ngozi tofauti.

Mama yao Donna ni nusu Mjamaica huku baba yake akiwa mzungu.

Lakini pindi waliposikia kuwa watapata mapacha, hawakufikiria kama wangeza watoto wasiofanana kabisa.

Mapacha Lucy na Maria enzi wakiwa watoto
Lucy mwenye macho ya blue anayeishi Gloucester na familia yake alisema: Ilikuwa na mshtuko kwake kwasababu vitu kama rangi ya ngozi huwa havionekani kwenye scans kabla ya kuzaliwa.”

Lucy na Maria wakiwa na familia yao
“Hivyo hakuwa na wazo iwapo tulkuwa tofauti sana.”

Mapacha hao wenye miaka 18, ni wa mwisho katika familia ya watoto watano wakiwemo Jordan, George na Chynna. “Kaka zetu na dada zetu wana ngozi ambayo ipo kati ya Maria na mimi,” aliongeza Lucy.

“Hakuna anayeamini kuwa sisi ni mapacha. Hata kama tukivaa sare, bado hatuonani kama ni mtu na dada yake, sembuse mapacha. Marafiki walitufanya hadi kuwaonesha vyeti vya kuzaliwa kuthibitisha.”
Chanzo: Mail Online & Mirror Online
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment