Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
SONY DSCKumekuwa na malalamiko mengi ya kwamba Polisi wanawaonea raia, siku chache zilizopita kulikuwa na story ya tukio la Polisi kususiwa maiti ya kijana mmoja hapa TZ smbspo watu waliosusia maiti hiyo walidai Polisi walihusika kusababisha kifo cha mtu huyo, safarii hii imetokea Kenya.
Katika kaunti ya Nyeri nchini Kenya kuna tukio lililotokea jana March 26 ambapo watu waliokuwa wakiomboleza walichukua mwili wa mtu mmoja na kwenda nao katika kituo cha Polisi cha Mkurueni  wakidai Polisi walihusika na kifo cha mtu huyo.
Waombolezaji hao walichukua mwili huo katika chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Nyeri na kuandamana hadi kituo hicho kwa madai mwanaume huyo alipigwa risasi na Polisi wa kituo hicho, walikutana na maafisa wa Polisi ambao walijaribu kuwazuia lakini waliwashinda nguvu na kuweka jeneza kwenye mlango wa kituo hicho na kuondoka.
Polisi waliwarushia mabomu ya machozi  ili kuwatawanya, baadaye walikubaliana hali ikakaa sawa ambapo ndugu wa marehemu huyo walikubali kuuchukua mwili na kwenda kufanya mazishi.
Kusikiliza story hiyo iliyoripotiwa na kituo cha K24 bonyeza play hapa chini…

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top