June 23, 2025 01:22:38 AM Menu
 

Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Kufuatia sintofahamu kati ya wapenzi wawili, Emmanuel Eribariki ‘Nay wa Mitego’, ambaye ni msanii wa Bongo Fleva na Siwema Edson juu ya mtoto wao mwenye umri wa miezi mitatu, mwanaume huyo amesema yupo tayari hata kwa vipimo vya vinasaba (DNA) ili kuthibitisha kuwa Curtis ni mtoto wake wa damu.

Siwema ambaye Nay anadai kumfumania kitandani akiwa na mwanaume mwingine mjini Mwanza hivi karibuni, alisema Curtis si mtoto wa Nay, bali wa mwanaume mwingine ambaye hata hivyo hamtaji.
 
Akizungumza na Gpl, Nay alisema katika mambo yanayomshangaza na kumfedhehesha ni pamoja na ishu ya mzazi mwenzake kuropoka kuwa Curtis si mwanaye, kwani anaamini hayo ni maneno ya hasira na yeye ataendelea kumpenda mtoto wake.

“Ujue najiuliza sana maana ya kuongelea hili jambo mitandaoni, kusema Curtis siyo mwanangu, kiukweli ninamuacha aongee anavyotaka lakini nasisitiza kuwa ninampenda sana mwanangu,” alisema Nay wa Mitego.
 
“Niko tayari kupigana hadi tone la mwisho ili mwanangu aweze kuishi kwa amani na upendo na wala sioni tena kama kuna haja ya kuyapa nafasi maneno ya mtandaoni kwa sababu naamini Curtis ni mwanangu na nipo tayari hata kupima DNA nikibaini siyo wangu  nitajua la kufanya,” alisema Nay.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro
25 Mar 2015

Post a Comment

 
Top