
Msichana huyo alisema alishauriwa na mama yake kuweka kiazi sehemu zake za siri kama njia ya uzazi wa mpango kuzuia asipate ujauzito.
Binti huyo amesema mama yake ndiye aliyemuonesha njia hiyo ya asili kwa maelezo kwamba kiazi kinapoingizwa sehemu za siri ni njia nzuri ya uzazi wa mpango.
Baada ya kupita wiki mbili alianza kulalamikia maumivu yasiyokuwa ya kawaida na kuamua kwenda clinic, baada ya kufanyiwa uchunguzi aligundulika mizizi inayochipua ikichungulia kutoka kwenye sehemu zake za siri, lakini kiazi hicho kiliondolewa bila kupata athari zozote katika njia yake ya uzazi.
Njia zisizo sahihi na hatari za uzazi wa mpango bado zinaendelea kutumika ulimwenguni kote hasa na mabinti wadogo wanaojihusisha na uhusiano wa kimapenzi kabla ya wakati.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Post a Comment
Post a Comment