Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Uzima na Ufufuo, Josephat Gwajima amejisalimisha kituo cha polisi kati kuhojiwa juu ya kutoa lugha chafu dhidi ya Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.

Mchungaji Gwajima anatuhumiwa kumkashifu na kumtukana hadharani Kardinali Pengo. 
 
Matusi hayo   ni  yale yaliyoonekana kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii  ambapo kuna sauti iliyorekodiwa na picha za video zikimuonyesha Mchungaji Gwajima akimkashifu na kumtukana kwa maneno makali Kardinali Pengo katika hali ambayo pia imewaudhi watu wengine.

Hata  hivyo, mapema  leo  Asubuhi, kipande cha  sauti   ya  Gwajima kilisambaa   katika  mitandao  mbalimbali  ya  kijamii  kikidai kuwa Gwajima angejisalimisha Polisi Jumatatu kwa kuwa kwa sasa yupo Arusha na kuwataka waumini wake kufika polisi Jumatatu bila kufanya vurugu.

Haijafahamika  mara  moja  sababu  zilizomfanya  mchungaji  huyo  Kujisalimisha  leo  Ijumaa.

Nimekuwekea  Kipande  hicho  hapo  chini  ambapo  Gwajima  anajitetea  ni  kwa  nini  Alitumia  lugha  hiyo.
Au  Ingia  Hapa kumsikiliza.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top