Home
»
tanzia
» Soma Chanzo cha Kifo cha BOSS wa Tip Top Connection ABDUL BONGE na Picha za Waliohudhuria Msibani Leo Ziko Hapa
KIFO cha mdau wa muziki nchini ambaye ni mwanzilishi na meneja wa kundi la Tip Top Connection, Abdul Shaban Taletale, kilichotokea Magomeni-Kagera jijini Dar es Salaam, jana jioni kimeendelea kuzua utata kufuatia mtuhumiwa wa mauaji mtu aliyetajwa kwa jina la Nassoro Idd kuingia mitini.
Akizungumza na mandao huu, Meneja wa Kundi la Tip Top Connection na mdogo wa marehemu, Hamisi Shaban ‘Bab Tale’, alisema siku ya tukio Abdul Bonge akiwa maskani ya Tip Top Connection iliyopo Magomeni-Kagera alifuatwa na kijana mmoja na kuambiwa rafiki yake aitwaye Nassoro Idd alikuwa akipigana na mkewe hivyo aliagizwa na mama yake Nassoro akamwite ili awasuluhishe.
Muda mfupi baada ya kwenda kwenye ugomvi huo zilirudi taarifa kuwa Abdul Bonge ameanguka na kupoteza fahamu.
Bab Tale alisema walimpeleka Hospitali ya Saint Monica iliyopo Manzese-Darajani lakini waliambiwa tayari ndugu yao alikuwa amepoteza maisha. Kufuatia tukio hilo Nassoro ametorokea kusikojulikana lakini mkewe anashikiliwa na jeshi la polisi.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa muda wowote kwenda Kijiji cha Mkuyuni kilichopo Matombo mkoani Morogoro baada ya polisi kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo na kuwakabidhi mwili huo.
(PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY / GPL)
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) afariki dunia18 Jan 20160
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Mhandisi Suleiman Said amefari...Read more ?
- Tanzia: Mwandishi wa 'Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe' afariki18 Jan 20160
Mwandishi maarufu wa tamthilia na kitabu cha ‘Ngoswe, Penzi Kitovu cha Uzembe’, Edwin Semzaba am...Read more ?
- Tanzia: Leticia Nyerere Afariki Dunia11 Jan 20160
Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia N...Read more ?
- PICHA: MWILI WA MAREHEMU CELINA KOMBANI WAWASILI NCHINI26 Sep 20150
Viongozi mbalimbali wakiwa katika uwanja wa n...Read more ?
- Picha Kutoka Msibani Nyumbani kwa Akina Banza Stone Sinza Dar…18 Jul 20150
Kulikuwa na stori ya uzushi mitandaoni na June 24 nikamfata nyumbani kwao Sinza na kwenye m...Read more ?
- MAJONZI: Mwanamuziki Banza Stone Afariki Dunia17 Jul 20150
Staa wa Muziki wa Dansi Bongo, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amefariki dunia mchana huu baada y...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment