Deogratias mongela/Ijumaa
MTOTO aitwaye Badru Muhidin mwenye umri wa miaka miwili, amepata pigo kubwa baada ya kukatwa uume wake kimakosa na babu yake aliyekuwa amempeleka kutahiriwa kienyeji huko Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Mwajuma Hussein ambaye ni mkazi wa Yombo jijini Dar, alisema aliishi na mwanaye peke yake bila baba yake kwani walitengana Juni mwaka jana baada ya kuishi bila kufunga ndoa kwa muda mrefu, lakini mara kwa mara alikuwa akimpeleka mwanaye nyumbani kwa wazazi wa mumewe kuwasalimia.
“Wiki iliyopita babu yake Eliyasa alimuomba ili wakakae naye kwa muda mfupi, baada ya muda mfupi walimtuma mtu akaniambia kuwa wameshamtahiri, nilishangaa sana kwa kuwa hawakunitaarifu juu ya uamuzi huo, nikaenda kumuona lakini wakawa wananikataza kumtazama sehemu za siri wakidai mila zao haziruhusu kwa kipindi cha mwezi mzima.
“Kutokana na shauku ya kutaka kuthibitisha hilo, siku hiyo nilipofika tu nilimchukua na kumtazama hilo eneo ndipo nikabaini kuwa alikuwa amekatwa katika kichwa, huenda huyo ngariba hakuwa mzoefu, kamfanyia kienyeji lakini wengine wakisema huenda walitaka kufanya mambo ya kishirikina,” alisema mama huyo.
Alisema baada ya kumkuta katika hali hiyo, alianza kuhangaika naye hospitalini kutafuta msaada, alipofika Temeke aliambiwa na madaktari.kwamba kijana wake alikatwa vibaya na hivyo analazimika kufanyiwa upasuaji ili kumnusuru.
“Madaktari watatu walimuangalia na kwa kuogopa kumuathiri zaidi, waliniambia niende Muhimbili, nimeumia sana, nahofia mwanangu akija kuwa mtu mzima atakuwa goigoi tu, asije akawa shoga baada ya kukata tamaa kwa hali iliyomtokea, japo wanasema kwa kuwa bado mdogo huenda ile sehemu ya ngozi itaota lakini ndiyo maumbile yake yatakuwa na jeraha, hatokuwa kama wanaume wengine.”
Babu wa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kufunguliwa shauri katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani kwa madai ya ukatili kwa faili namba UKATILI WA MTOTO/MBL/RB/2251/2015 4/3/2015.
Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
Je Umezisoma Hizi?
- Tetemeko Lililotokea Jana Katika Mikoa Ya Kanda ya Ziwa Limeua Zaidi ya Watu 10 na Kujeruhi Wengine 12011 Sep 20160
Tetemeko la ukubwa wa mtikisiko wa kipimo cha Ritcher 5.7 limetokea katika mikoa mitatu nc...Read more ?
- Msafara wa Makamu wa Rais, Samia Suluhu wapata ajali Mtwara.09 Sep 20160
Msafara wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani, Mama Samia Suluhu Hassan ambao uliku...Read more ?
- Polisi Washuhudia Majambazi Yakitwangana Risasi.......Zakamatwa Shehena za Silaha na Vifaa vya Uhalifu06 Sep 20160
WATU watatu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi wa kutumia silaha, ambao wamehusika kufanya matukio ...Read more ?
- Askari Magereza Atiwa Mbaroni Kwa Kuingia Wodini Akiwa Amelewa na Kisha Kuanza Kufyatua Risasi28 Aug 20160
POLISI mkoani Rukwa inamshikilia askari Magereza, Cleophas Chapaulinge kwa kosa la kulewa na k...Read more ?
- Polisi Mwingine Auawa Kwenye Mapambano Makali na Majambazi Huko Mkuranga27 Aug 20160
Ilikuwa ni kama filamu ya askari na maadui wakati askari wa Jeshi la Polisi walipopambana na wat...Read more ?
- RC Makonda: Polisi Mkikuta Mtu Yeyote Msituni Pigeni bila Huruma.......Haki za binadamu Wakiwauliza Waambieni waje Kwangu26 Aug 20160
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ameliagiza Jeshi la Polisi kuwagonga na kuwapiga wah...Read more ?
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment
Post a Comment