Share this PostPin ThisShare on TumblrShare on Google PlusEmail This
MAMBO yanazidi kunoga ndani ya safu hii ya Sindano 5 za moto, kutokana na maombi yenu, leo tumemleta kwenu mwigizaji Jeniffer Kyaka ‘Odama’, tiririka naye:
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Jeniffer Kyaka ‘Odama’.
Paparazi: Mambo vipi Odama! Tuanze moja kwa moja na swali la kwanza, hivi kwa sasa una mpenzi? Mbona hatumjui?Odama: Mambo poa! Mpenzi ninaye, nampenda muda bado wa kumuanika.Paparazi: Ulishawahi kuchangia bwana na mwanamke mwingine katika maisha yako?
Odama: Hapana, sina kumbukumbu hiyo.
Paparazi: Hadi leo hii unaweza kukumbuka idadi ya wanaume ambao umewahi kutoka nao kimapenzi?
Odama: Nakumbuka, kama mtu hukumbuki idadi basi lazima utakuwa una kichaa. Nakumbuka kwa sababu idadi ni ndogo, ila hapa sitataja idadi yao.
Paparazi: Hivi baba mtoto wako ni nani hasa au ndiye uliyenaye hadi sasa?
Odama: Hilo liweke kapuni kwa sasa, nitalizungumza ‘next time’.Paparazi: Inasemekana wewe ni miongoni mwa warembo ambao wanaoongoza kwa kutongozwa Bongo Movies, ni kweli?
Odama: Hiyo kawaida kwa mtoto wa kike, nadhani sipo peke yangu.

Je, Una Habari,Picha,Tangazo,Makala,

Hifadhi blog hii kwenye simu yako ili upate habari zote kwa urahisi zaidi

Facebook Blogger Plugin by Kibonajoro
http://www.facebook.com/kibonajoro

Post a Comment

 
Top